Kikao Baina ya Waziri Mkuu (MUSO) pamoja na Wawakilishi wa Wanafunzi

Serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe Kupitia ofisi ya Waziri Mkuu inawatangazia Viongozi wa vitivo na Skuli (FR’s na SR’s) waliopo Chuoni kuwa, Kesho Jumatano tarehe 01/08/2018 kuanzia ya saa Moja kamili Jioni mpaka saa mbili na nusu usiku (07:00 – 08:30 pm) kutakua na kikao cha viongozi tajwa hapo juu na Waziri mkuu wa serikali ya Wanafunzi MUSO, mahali ni ofisi ya Serikali ya wanafunzi .

Tarehe 02/08/2018 Saa Moja kamili Jioni mpaka saa mbili na nusu usiku (07:00 – 08:30 pm) watakutana wawakilishi wote wa madarasa (CR’s) na Waziri mkuu darasa la CR 9.

Lengo la vikao hivyo ni kujadili mambo muhimu yahusuyo taaluma na changamoto zinazowakumba wanafunzi ili kuweza kuzikabili kwa wakati, aidha ofisi ya waziri mkuu itapokea changamoto, ushauri pamoja na mapenekezo mbalimbali.

MUNGU IBARIKI MUSO, MUNGU IBARIKI CHUO KIKUU MZUMBE.

 

UPATAPO UJUMBE HUU, MTAARIFU NA MWENZAKO

USISAHAU KUTUTEMBELEA KWENYE MITANDAO YETU YA KIJAMII  twitter @mzumbe _media, Instagram @mzumbe_media, Facebook – Mzumbe Media

 

………………………..

Zephania J. Sane

Waziri Mkuu-MUSO – 0714 29 60 10

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *