Uchukuaji wa Vyeti vya Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO)

Serikali ya Wanafunzi (MUSO) kupitia Wizara ya Habari, Teknolojia na mawasiliano Chuo kikuu Mzumbe inawatangazia Viongozi wote wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe (MUSO) walioshika nyadhifa mbalimbali za uongozi kwa mwaka wa masomo 2017/2018 (Student Representative Council 2017/2018) kuwa Siku ya Jumanne tarehe 17/07/2018 kutakua na zoezi la ugawaji wa vyeti vya uongozi, aidha zoezi hilo litafanyika katika ofisi ya serikali ya wanafunzi (MUSO) kuanzia majira ya saa Sita Kamili mchana mpaka saa Tisa na Nusu Jioni, na litaendelea tena siku ya Jumatano tarehe 18/07/2018.

Tafadhali waheshimiwa wote mnaombwa kuzingatia muda wa zoezi.

MUHIMU: Fika ukiwa na kitambulisho chako cha chuo, hakutakua na utaratibu wa kuchukiliana vyeti.

UPATAPO UJUMBE HUU, MTAARIFU NA MWENZAKO

USISAHAU KUTUTEMBELEA KWENYE MITANDAO YETU YA KIJAMII  twitter @mzumbe _media, Instagram @mzumbe_media, Facebook – Mzumbe Media

 

………………………..

Christopha Mbinda

Wizara ya Habari, teknolojia na Mawasiliano (MUSO) – 0767 973 853

2 Replies to “Uchukuaji wa Vyeti vya Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *