Baraza la wanafunzi lafanyika likiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mh. Mzakiru Twalibu

Baraza hili la Wanafunzi limefanyika katika Ukumbi wa Samora tarehe 21/09/2019, likiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi 2019/2020 Mh. Mzakiru twalibu  pamoja na katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Bi. Winfrida Gavana. Baraza lilihudhuliwa na wanafunzi kutoka shule na vitivo vyote vilivyopo muhula wa kusepetua “Staggered Semister” ambao waliweza kushauri na kutoa mapendekezo yao pamoja na kupokea mrejesho kutoka katika Serikali ya Wanafunzi. Akizungumza na Wanafunzi Mh. Rais wa Serikali ya Wanafunzi MUSO alitangaza juu ya taarifa ya kuanzishwa mfumo wa Ki-electroniki wa kukata Bima ya Afya ya NHIF ambao utaanza kutekelezwa oktoba mwaka huu na kupisha mfumo wa zamani wa kutumia karatasi. Pia aliwaelekeza kinagaubaga wanafunzi juu ya matumizi sahihi rasilimali za chuo, kudumisha amani pamoja na kusoma kwa bidii. Aidha wanafunzi wameipongeza serikali kwa juhudi chanya zenye maslahi mapana kwa MUSO nzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *