Baraza Jipya la Mawaziri la Serikali ya Wanafunzi MUSO 2018/2019

Rais wa Serikali ya Wanafunzi MUSO, Mh. Mzakiru Twalibu, mnamo Tarehe 23 Augusti 2019 aliteua baraza Jipya la Mawaziri, ambapo Baraza linaundwa na Wizara sita (6) ambazo ni, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya na Malazi, Wizara ya Habari na Michezo, Wizara ya Mambo ya ndani, Ulinzi na Usalama,  Wizara ya Katiba, Haki, Maswala ya Bunge na Utawala Bora, Pamoja na Wizara ya Elimu na Masuala ya Mikopo. Baraza lina Jumla ya Mawaziri sita (6) na Manaibu Waziri tisa (9), Wanaofanya idadi ya Mawaziri kuwa Kumi na Tano (15). Pongezi kwa Mh. Rais, na Mawaziri Makini walioteuliwa, Wanafunzi Wa chuo Kikuu Mzumbe wanatarajia Mengi kutoka Kwenu