MUST-SA watoa huduma za TEHAMA bure kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe

Umoja wa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi na teknolojia Chuo kikuu Mzumbe Ujulikanao kama “Mzumbe University Science and Technology Student’s Association” (MUST-SA) umeendesha tukio la kutoa huduma zinazohusiana na masuala ya TEHAMA bure kwa wanafunzi na wafanyakazi ndani ya Chuo kikuu Mzumbe. Huduma hizo hutolewa kila siku ya Jumamosi ya Kwanza ya kila mwezi, huduma ambazo zinatolewa na umoja huo hujumuisha Marekebisho ya Kompyuta, Simu za Mkononi pamoja na kuwasaidia wanafunzi jinsi ya kutumia mifumo mbalimbali inayopatikana chuoni hapa.