Tangazo la kusaini fedha ya kipindi cha Mafunzo kwa Vitendo (Field)

Serikali ya Wanafunzi (MUSO) kupitia Wizara ya Mikopo Chuo Kikuu Mzumbe inawahimiza wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na wapili ambao wanaanza mafunzo ya vitendo (Field) mwezi wa nane na wale waliohakiki fedha zao za mafunzo ya vitendo (Field)  ambao ni wanufaika wa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini (HESLB)   kuwa Siku ya Ijumaa tarehe 20/07/2018 kutakua na zoezi la kusaini fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Field), aidha zoezi hilo litafanyika eneo la bohari kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa kumi  kamili jioni. Pia kwa wanafunzi wote wanaoendelea na masomo ambao wametuma maombi ya kupatiwa mikopo na bodi ya mikopo (HESLB)wakiwa wanaendelea na masomo hapa chuoni kuwa wanatakiwa kufika bohari siku na muda tajwa hapo juu ili kuorodhesha majina yao kwenye karatasi maalumu kwa ajili ya kuyapeleka matokeo yao ya     kitaaluma bodi ya mikopo.

UPATAPO UJUMBE HUU, MTAARIFU NA MWENZAKO

USISAHAU KUTUTEMBELEA KWENYE MITANDAO YETU YA KIJAMII  twitter @mzumbe _media, Instagram @mzumbe_media, Facebook – Mzumbe Media

 

………………………..

Omary Zubery

Wizara ya Mikopo (MUSO) – 0713 581 350

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *