Mahafali ya 18 Chuo Kikuu Mzumbe kampasi kuu yafanyika

Mahafali ya 18 ya wahitimu kwa ngazi zote za elimu Chuo Kikuu Mzumbe yamefanyika jana tarehe 22/11/2019. Mahafali haya yamefanyika Kampasi kuu ya Chuo kikuu Mzumbe na kuhudhuliwa na Mgeni rasimi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samata. pamoja na wageni mbalimbali akiwepo Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda, na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (RC) Loatha sanare. Ratiba ya Mahafali kwa kampasi ya Mbeya itakuwa ni tarehe 29/11/2019 na Kampasi ya Dar- es – salaam itakuwa ni tarehe 6/12/2019. Nyote mnakaribishwa

Tujifunze kwa maendeleo ya watu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *