Rais wa Serikali ya wanafunzi (MUSO) 2018/2019 akiapishwa

Rais mpya wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe (MUSO) mheshimiwa Millah Mng’ong’o akiapishwa kiapo cha utumishi baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huru wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Aidha tukio hilo la kuapisha viongozi wapya liliongozwa na wakili Ndugu. Innocent Mgeta ambae pia ni mhadhiri kutoka kitivo cha Sheria chuo kikuu mzumbe. Pia tukio hilo lilihudhuriwa na Makamu mkuu wa chuo Prof. Lugano Kusilika akiongozana na Makamu mkuu Msaidizi Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na Makamu mkuu msaidizi taaluma Prof. Nyamsogoro. Mbali na viongozi tajwa hapo juu pia wakuu wa vitivo na skuli, wakuu wa idara, wafanyakazi wa chuo kikuu Mzumbe, wahadhiri pamoja na wanafunzi wote pia walihudhuria tukio hilo.